Wednesday, May 30, 2012

Kim Kardashian: NIMEIBIWA MIWANI AMBAYO THAMANI YAKE HAKUNA KITU KINACHOWEZA KUFANANISHWA

 Mwanamitindo,muigizaji,na mjasiria mali,Kim Kardashian, Juzi ijumaa ameibiwa miwani yake iliyokuwa ndani ya begi maeneo ya airpport akiwa anatokea Ufaransa na kudai kuwa hakuna kitu kinachoweza kulipa thamani yake.

Amesema kuwa miwani hiyo ya jua aliachiwa na baba yake Robert Kardashian kabla hajafariki na huwa anayavaa pindi akiwa kwenye matukio maalum tu.
Kupitia akaunti yake ya twitter Kardashian baada ya kugundua ameibiwa ali twit ""Very disappointed in British Airways for opening my luggage & taking some special items of mine! Some things are sentimental & not replaceable."
Pole sana Bi. dada.

Tuesday, May 29, 2012

Nas - Daughters

JUSTIN BIEBER MIKONONI MWA SHERIA KWA KUMSHAMBULIA PAPARAZI

Justin Bieber juzi jumamosi yamemkuta yale yaliyomkuta Diamond platinum wa TZ kwa kumshambulia paparazi kisa mdaku huyo alitaka kumpiga picha.
Kesi hiyo kwasasa ipo mikononi mwa polisi kwa uchunguzi mjini California..

MJOMBA MKUDE: MKALI MWENYE DAMU YA HIP HOP HUYU HAPA

Davis Alfred Mkude a.k.a Mjomba Mkude, ni mkali anayeibukia upande wa muziki wa kizazi kipya atoka na singo ya kwanza iitwayo Sina Pesa.

Mjomba Mkude anasema kuwa hiphop ipo ndani ya damu tangu kitambo na anaamini ataitendea haki siku zote.
Amefunguka kuwa ngoma zipo nyingi na kali zinakuja kutoka kwake hivyo wadau wa hipiT-hiphop wakae tayari.
Kuhusiana na kuchanganya muziki na kazi jamaa ametiririka kuwa kila kitu kina nafasi yake.

Ngoma hiyo ya Sina Pesa imeanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya redio na pia unaweza kuipata kwenye mitandao mbalimbali ikiwemo blog hii.

All the best jombaaa.

Monday, May 28, 2012

Shetta ft Diamond - Nidanganye (Official Video)

Take It To The Head (Explicit)-DJ Khaleed,Rick Ross,Chris brown ,Nicki Minaj & Lil wayne

Nicki Minaj - Right By My Side (Explicit) ft. Chris Brown

MARY J. BLIGE AKWEPA KULIPA DENI BENKI

Malkia na gwiji wa miondoko ya Soul, mdada Mary J. Blige  yupo kwenye wakati mgumu baada ya kuingia kwenye skendo ya kukwepa kulipa deni benki lenye thamani ya dola za kimarekani 250,000 kutokana na mkopo waliochukua mwaka jana kwaajili ya kusaidia maendeleo ya wanawake kupitia foundation yake na Steve Stoute.Benki imesema iliwapasa kulipa deni desemba 2011 lakini hela iliyolipwa ni dola 368.33 tu.

Pia foundation hiyo inashukiwa kwa kutowalipa wasanii kadhaa walioitwa ku 'perform' kwenye 'fund raising' fulani huko mtoni.

MO' CHEDDAH APOTEZA DIRA KWENYE SINGO YAKE MPYA YA 'LOUDER'

Mkali kutoka Nigeria Bi. dada Mo'Cheddah, POP DIVA, Ameonekana kushuka badala ya kupanda katika tasnia ya muziki, hususan baada ya kutoa ngoma yake iitwayo 'LOUDER'.

Kwenye ngoma hii auto tune zimekuwa too much kiasi cha kupoteza ile melody yake ambayo imezoeleka masikioni mwa fans wake.
Kutokana na hayo, wataalamu wa mambo wanatia shaka juu ya ujio wake huo mpya baada ya kimya kingi sana kuwa anaonekana kushuka kiaina.
Ingawa hatuwezi jua lengo la Cheddah,labda keshagundua soko lake jipya.
Video ya ngoma hiyo imefanyika nchini Afrika ya kusini chini ya director Brandon, na humo Mo' ameonekana kwenda nje ya uafrika kitu ambacho kinaweza kupotezea tena umaarufu wake.

Sina pesa-Mjomba Mkude ft.Man Keno (prod...

Gonga hapa umsikie mwana kwa mara ya kwanza kabisa kwa hewa

 Sina pesa-Mjomba Mkude ft.Man Keno (prod... in Hulkshare: