Tuesday, December 4, 2012

P. FUNK 'MAJANI' ASEMA TEKNOLOJIA IMEATHIRI MAUZO YA ALBAM BONGO FLEVA

Unapoongelea muziki wa Bongo Fleva huwezi kuacha kutaja jina la mtayarishaji 'producer' wa muziki huo Paul Mathyse Maarufu kama P. Funk kutoka Studio za Bongo Records. Mkali huyo amefunguka kuwa mauzo ya albamu za muziki huo umeshuka sana kwa hivi sasa. Amebainisha kuwa kipindi cha miaka ya 2001  wasanii walikuwa wakiuza hadi zaidi ya kopi laki tatu,huku akitolea mfano wa albam ya starehe ya Feruz jinsi ilivyofanya vizuri. P. ameweka wazi kuwa sababu kubwa inayosababisha kushuka kwa mauzo ya albam ni kukua kwa teknolojia ya habari ambapo redio stations zinazo piga muziki huo sikuhizi zimekuwa nyingi, mitandao ya kijamii ikiwemo You tube n. k. hivyo msikilizaji anaweza kupata muziki wowote anaouhitaji kwa muda wowote kuliko zamani ambapo wasikilizaji wengi walikuwa wakitegemea tapes. Kwa upande wake anaona kuwa teknolojia inasaidia kuwasogeza wasikilizaji hivyo kutanua soko la muziki.
Mkali P. Funk ameyasema hayo leo kupitia mahojiano yake aliyofanya katika kipindi maarufu cha XXL cha Clouds FM katika segment ya 255.

0 comments:

Post a Comment