Wednesday, November 20, 2013

A.Y AAMUA KUTIMIZA NDOTO YA KUWA RUBANI,AINGIA SHULE RASMI.

Ni ngumu sana kwa mtu maarufu, mwenye hela na uwezo wa kilakitu anchohitaji kuamua kutimiza ndoto
aliyokuwa nayo kitambo. Lakini hii inaenda kutokea kwa mkali A.Y 'Ambwene Yesaya' ambaye ameamua kurudi Chuo na kufanya kitu ambacho alikuwa anakitamani long time kitambo. Lakini hii haimaanishi kuwa mchizi anaacha muziki. Kwasasa A.Y amesha lipa ada ya hiyo kozi katika  Chuo cha Mafunzo ya Urubani cha ‘Mosswood Aviation Academy’ kilichopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) na anatarajia kuanza masomo Januari 2014.Amefunguka hayo kupitia Mwananchi Hili ni bonge la concept kutoka kwa mchizi na ni mfano bora. All the best bro.