Sunday, July 24, 2011

Langa (rais wa mateja)aachana na vijiti

Mchizi na mkali wa bongo hiphop Langa ambaye kwa mara ya kwanza alisikika hewani akitokea kwenye cocacola pop idol ametangaza rasmi kupitia vyombo vya habari mbalimbali vya nchini kuwa ameachana na madawa ya kulevya.

Mchizi kafikia uamuzi huo kutokana na ukweli kwamba yamemlostisha kinoma kiafya hadi kisaikolojia. Amesema amefikia maamuzi hayo ya kujitangaza ili iwe kama lesson kwa vijana wengine wa mlengo huo.

Kimsingi mchizi alifunguka kuwa kutokana na ushauri kutoka kwa watu wake wa karibu ndipo alipoamua kwenda kwenye ushauri nasaha.

Yote kwa yote mchizi karudi rasmi kwenye gemu na kwa mujibu wake mwenyewe angependa umuite RAIS WA MATEJA. Duuu; Tumsikilizie ujio wake mpya (reloaded) hv karibuni.

2 comments: