Saturday, September 8, 2012

COLLINS 'MO LOVER' KICHWA KIPYA BONGO, ATOKA NA "NILIKUPENDA"

Kutoka studio ya AM Records chini ya mhunzi wa sauti Manecky, anapatikana mchizi huyu hapa
Collins a.k.a Mo'Lover akiwa amemshirikisha Drama boy wamedondosha ngoma kali ambayo kwangu mimi naona kama ni 'Good Start n good staff'.Baada ya kunitumia hii ngoma nikaona ni vyema nikikudondoshea na wewe uisikie kisha ujipakulie.

Saturday, September 1, 2012

MR. FLAVOUR ABURUZWA MAHAKAMANI NA WAGHANA KWA WIZI WA WIMBO

Mkali kutoka Nigeria Flavour N'ababia maarufu kama Mr. Flavour ameburuzwa mahakamani na wasanii ktuka Ghana wajulikanao kama Wutah kwa tuhuma za kuiba wimbo wao wa mwaka 2008 uitwao 'Kotosa'. Kwa mujibu wa waghana hao 'Wutah' wameutaja wimbo mpya wa Flavour uitwao 'kwarikwa' kuwa ni 'kopi' ya wimbo wao uitwao 'kotosa' ambao
waliuachia hewani 2008. Wanamtuhumu Flavour kwa kuiba chorus,rhythm na tempo ya wimbo wao huo bila idhini wala makubaliano yoyote.Meneja wa Flavour, Benjamin, amekataa kuongea chochote juu ya tuhuma hizo kwasasa. Flavour ambaye Jina kamili ni Chinedu Okoli, kwasasa yupo chini ya 2nite entertainment. Hapa chini ni video yake ya 'kwarikwa' akimshirikisha Fally ipupa. Jaribu kuzitofautisha hizi ngoma hapa chini WUTAH KOTOSA

Powered by mp3skull.com FLAVOUR - Kwarikwa ft. Fally Ipupa | Jaguda.com

Powered by mp3skull.com