Monday, November 19, 2012

SNOOP DOGG ATAKA KUINUNUA CELTIC NA KUMSAJILI BECKHAM

Mkongwe na mkali wa Rap kutoka nchini Marekani, Snoop Dogg ameweka wazi nia yake ya kununua hisa ya klabu ya mpira wa miguu ya Celtic ya Uingereza. Snoop ambaye amewahi kupigwa marufuku kuingia nchini uingereza kutokana na makosa yanayohusishwa na madawa ya kulevya na matumizi ya silaha za moto, ameweka wazi kuwa ameshafanya mazungumzo na rafiki yake kiungo mkali wa LA Galaxy David Beckham ili akipige katika klabu yake pindi akikamilisha taratibu. Snoop amefikia wazo hilo baada ya kuvutiwa na kocha wa Celtic, Neil Lennon, mara baada ya kuichapa Barcelona kwenye mashindano ya klabu bingwa ulaya yanayoendelea. "Sio kitu kipya  kwa supastaa wa hiphop kuwekeza kwenye michezo,lakini ni kitu kipya kwa supastaa wa hiphop kuwekeza kwenye football" alisema Snoop kupitia 'The Scottish Daily Record'. Kwaupande wangu naona ni bonge la wazo kwa mkali huyu. All the best bro.

0 comments:

Post a Comment