Tuesday, November 27, 2012

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

Yule mkali wa sanaa ya vichekesho na bongo fleva Hussein Ramadhani Mkieti,maarufu kama Sharo milionea amefariki dunia jana majira ya saa mbili usiku katika kijiji cha Lusanga-muheza,Tanga kutokana na ajali ya gari iliyotokea akiwa njiani akielekea nyumbani kwao Muheza.
akitokea Dar ea salaam. Kamanda wa Tanga Bwana Costantine Masawe amethibitisha kutokea kwa kifo cha msanii huyo. Kamanda Masawe  amesema ajali imetokea baada ya gari dogo lenye usajili na. T478 BVR Toyota Harrier lililokuwa linaendeshwa na marehemu kuacha njia na kuingia mtaroni na kusababisha umauti huo. Mpaka sasa mwili upo hospitali teule ya muheza Tanga na mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano wiki hii.  R.I,P Sharo Milionea, we realy Gonna mic u Bro.

0 comments:

Post a Comment