Saturday, January 19, 2013

T.I AELEZEA UWEZO WAKE KATIKA GAME, ASEMA ALBAM YAKE MPYA YATHIBITISHA HILO

Mkali kutoka ATL, T.I amesema kuwa watu wenye shaka na uwezo wake kwenye gemu bado hawamjui fresh. Akiongea na DX T.I amesema kuwa hakuna kitu kibaya kama kuambiwa huna uwezo wa kufanya kitu ambacho uliumbwa ili ukifanye. Kwa miaka 11 ndani ya gemu hadi hivi sasa bado kuna watu hawaamini uwezo wa T.I. Na hiki ndicho kitu kinachomuumiza kichwa. Kupitia albamu yake mpya, Trouble Man: Heavy Is the Head T.I anataka kuwaprove wrong hao wasioamini uwezo wake.
Na katika hatua nyingine imeripotiwa kuwa T.I amemaliza mkataba wake na label ya Atlantic Records na kwasasa ni free agent, na ameweka wazi kuwa anahitaji kusaini label/record deal mpya kwa dola milioni sabini na tano ($75 million) na tayari Dr. Dre na Jay-z wameonesha nia ya kumsainisha mkali huyu kupitia Interscope na Roc Nation.

0 comments:

Post a Comment