Tuesday, February 12, 2013

Rapper Common asema Apatikane Papa Mweusi Baada ya kutangaza kujiuzulu kwa Papa Benedict XVI

Rapper Common, ameonesha wazi hisia zake za kuhitaji kupatikane Kiongozi mpya wa wakatoliki duniani ( Papa ) mwenye asili ya kiafrika mara baada ya papa Benedict XVI kutangaza kujiuzulu wadhifa huo ifikapo tarehe 28 februari 2013. Rapper huyo ameongea hayo alipokuwa ameulizwa na TMZ juu ya kujiuzulu kwa papa Benedict xvi na mtazamo wake juu ya hilo. Na alipoulizwa nani anaweza kukaa kwenye nafasi hiyo Common hakusita kumtaja Kadinali Peter Turkson kutoka Ghana kuwa anaweza kushika nafasi hiyo. "electing a black Pope would be a beautiful thing" alisema Common.

0 comments:

Post a Comment