Tuesday, October 29, 2013

CHRIS BROWN AACHIWA BAADA YA KUSOTA JELA MASAA 36

Hatimae Chris Brown ameachiwa huru baada ya kusota jela kwa zaidi ya masaa 36 kutokana na shambulio alilolifanya kwa mtu nje ya Night Club.
Breezy na Bodyguard wake walikamatwa Juzi Jumapili asubuhi baada ya kumchapa jamaa aliyefahamika mahakamani kwa jina la Parker Adams mwenye umri wa miaka 20. Jamaa amesema mahakamani kuwa alikuwa anataka kupiga picha na Breezy ghafla akastukia akitupiwa sumbwi na breezy.
Kwa mujibu wa Mahakama Chris Brown na Bodyguard wake wamekutwa hawana hatia na wameachiwa huru.ila wameamriwa kurudi mahakamani Novemba 25 na kukaa umbali wa yard 100 na jamaa aliyewashtaki.

0 comments:

Post a Comment