Monday, October 28, 2013

Kwanini Jay-Z na NAS ni mfano wa kuigwa kwenye Hip hop???

Wakali ambao wana historia za kipekee kwenye ulimwengu wa Hip hop Nasir Jones Escoba 'Nas' na Sean Carter 'Jay -Z' ni mfano mzuri wa kuigwa katika ulimwengu wa Hip hop. 
2005- Ulikuwa ni mwaka ambao kulikuwa na bifu kali ya Jay-Z na Nas katika ulimwengu wa Hip hop. Baada ya Jay-Z kumponda Nas kwenye tamasha la Summer Jam 2001 na kutoa album aliyoiita 'Take over' to the world, Jay Z na Nas waliingia kwenye vita kali ya mashairi,kama vile Take over ya Jay-Z vs Ether ya Nas, Ether vs Super Ugly, Super ugly vs The Last Real Nigga Alive na Blue print2.  Kilichofurahisha katika bifu ya Jay Z na Nas ni kwamba bifu ilitengeneza Great Music na haikuwa kama bifu zinazo ibuka miaka ya hivi karibuni. Na bifu ya Jay na Nas ndo bifu ambayo kwa upande wangu nadhani inafaa kuwa mfano kwa wasanii wasasa wa Hip hop.
Mnamo October 27, 2005, katika tamasha la Powerhouse Concert  lililoandaliwa na  kituo cha radio 105.1 ndipo ambapo bifu ya Jay-Z na Nas ilikua officialy squashed pale Nas alipo tokea kwenye show ya Jay-Z bila kutarajiwa. Na hapo kwa makusudi jina la show likabadilika na kuitwa 'I declare War' yani 'Natangaza Vita'. Watu wengi mashabiki wa Jay walitegemea Jay angejipanga kwa mashairi ya vita dhidi ya adui yake 'Nas'. Badala yake Jay-Z aligeuka na kupanda stejini akiwa na adui yake Nas na kuperform ngoma ya 'Dead Presidents' na 'The World is Yours'. Baada ya Performance Jay na Nas wakapeana mikono na ukawa ndo mwisho wa Bifu yao. Hapo ndipo unapata picha kuwa ile 'I Declare War' ni kinyume cha 'I Declare Peace'.
Mnamo Januari 2006,  Jay-Z na Nas  wame make headlines baada ya Jay kumsaini Nas kuingia Def Jam wakati Record label ikiwa chini ya Hov. 'Jay-Z'.  Nas aliendelea kushirikiana na Jay  katika  album ya Hip hop is dead  kupitia ngoma ya 'Black Republicans' na kwa mara nyingine mwaka 2007 wametoa ngoma ya 'Success'.
Huu ni mfano mzuri kwa wana hip hop wa sasa kujifunza namna ya bifu za kujenga.

0 comments:

Post a Comment