Monday, October 28, 2013

CHRIS BROWN ATIWA NGUVUNI KWA KUMTUPIA MASUMBWI MTU

Mkali Chris Brown 'Breezy' Jana mida ya saa 4 asubuhi amekamatwa na makachero kwa kosa la kumchapa makonde jamaa mmoja ambaye inasemekana hawajuani. Taarifa zilizopatikana kutoka mtandao wa TMZ zinasema Mchizi Breezy aliingia kwenye majibizano na mchizi mwingine nje ya Hotel, huku na huku Breezy si  akamrushia jamaa Konde la uso na inasemekana aliyepigwa hajarudishia mashambulizi. Breezy alikamatwa na kutupwa sero akiwa na Bodyguard wake.
Breezy bado yupo kwenye maangalizi ya kesi ya kumshambulia Rihana na ameongeza ishu nyingine. By the way kinachonishangaza kwa Breezy ni kwamba hivi alimuajira Bodyguard afnye kazi gani iwapo mpango wa ngumi anausimamia mwenyewe. LOL!!!

0 comments:

Post a Comment