Saturday, June 16, 2012

BAADA YA KUMWAGWA TIP - TOP, DOGO JANJA AFUNGUKA. ASEMA MUNGU NDO ATAKAYEMLIPA

Wiki hii imekuwa hot kwa Dogo Janja Baada ya mtu pekee aliyemleta Dar na kumuunganisha na Kundi la Tip-Top, Madee, kumtosa rasmi na kumrudisha kwao Ngarenaro, A.city.
Yameongelewa mengi na Madee pamoja na Babu Tale ambaye ndio msimamizi wa Kundi kuhusu Dogo,lakini Leo Dogo kafunguka kuwa Madee sio 'Binadamu' kutokana na dhuluma ambazo amekuwa akimfanyia kwa kipindi chote alichoweza kuwa katika kundi. Amesema kuwa hajawahi kugusa hata senti moja ya albam yake na show zote alizopiga alikuwa anapewa hela ndogo sana,mfano show ya milioni 1 alikuwa akipewa laki mbili tu. 
Kwasasa Dogo yupo homa Arusha na kwa mujibu wa Mma yake mzazi ni kuwa Dogo kapokelewa na wasanii wakali wa Arusha akiwemo JCB kitu ambacho hakukitegemea. Kwa upande wa Baba mzazi wa Dogo amesema kuwa wanaangalia namna ya kuweza kutafuta haki za Dogo.
Kuhusu shule Dogo amesema hakuacha shule ila anafanya taratibu za kuhamia Arusha. Ila kubwa kabisa amesema anaamini Mungu ndiye mlipaji wa mambo yote aliyofanyiwa na Madee/Tip-Top kwani anaamini haki ya mtu haipotei.
Haya yote yamefikia hapo baada ya Madee pamoja na Babu Tale kumshutumu Dogo kuwa amekuwa mtoro wa shule na msumbufu,kitu ambacho kimekanushwa na mama mzazi wa Dogo baada ya kuwasiliana na walimu wa Dogo.





0 comments:

Post a Comment