Saturday, June 16, 2012

YOUNG D AMWAGA CHOZI LIVE REDIONI BAADA YA KUKUMBUSHWA MWANZO WAKE WA MUZIKI

Young D, Young Dar es salaam,Young rapper, Dee Leo mchana amemwaga chozi Live redioni katika kipindi cha Bongo fleva cha clouds FM baada ya presenter Adam Mchomvu, Baba Jonii,kum surprise kwa kumsikilizisha clip ya interview yake ya kwanza kabisa alipoanza muziki.
Akiongea akiwa katika hali ya kwikwi ya kilio, Dee amesema kuwa mara ya mwisho kulia ilikuwa baada ya kifo cha baba yake na hii ya leo imemkumbusha vitu vingi sana vya nyuma kiasi ya kwamba ameshindwa kujizuia na kumfanya asiendelee na interview hiyo na kumuacha Mchomvu akiongea na mtu aliye ambatana na Dee ambaye anamfahamu vizuri.

0 comments:

Post a Comment