Sunday, December 23, 2012

NAS ATAKIWA KULIPA $MILION 10 KWA KUTOTOKEA KWENYE TAMASHA ANGOLA

December 2011,promota wa American concert,Patrick Allocco alitekwa na mapromota wa Angola baada ya Nas kutotokea kwenye tamasha la mwaka mpya nchini Angola ambapo tayari alishalipwa. Promota huyo amesema kuwa alitekwa ili aweze kuwarudishia mapromota hao kiasi cha pesa zilizotolewa kwaajili ya tamasha hilo. Huku na huku Promota huyo aliweza kuachiwa huru mwezi february 2012. TMZ  
inasema kuwa kwamujibu wa sheria promota Alloco amemfungulia kesi Nas kwa madai ya kutaka kulipwa dola za kimarekani milioni kumi ($10,000,000) akidai kuwa kwa siku 50 alizokaa kama mateka ameathirika kisaikolojia,kimwili na kifedha pia.
Kwa upande wake Nas alipohojiwa March 2012 alisema kuwa alitumika kama 'scapegoat' yani mtu anaye hukumiwa au adhibiwa kwa makosa ya wengine. Kesi imefunguliwa Ijumaa juzi tarehe 21 Dec.2012.

0 comments:

Post a Comment