Friday, August 9, 2013

50CENT HAYUMO KWENYE LIST YA UBABA KWENYE CHETI CHA KUZALIWA CHA MWANAE WA DAMU

Mkanganyiko ulitokea kwa 50Cent pindi alipotiwa nguvuni kwa kosa la kushambulia baada ya kumchapa demu wake wa zamani Daphne Joy mwezi uliopita. 50 alikana mashtaka na aliachiwa, lakini kitu cha kushangaza ni kwamba inawezekana mchizi akawa na mtoto na Bi.dada Daphne Joy ambaye hakuwahi kuweka wazi. Mwanasheria kutoka jiji la L.A amefunguka kuwa 50 na Daphne Joy wana mtoto kwa mujibu wa maelezo ya tukio la shambulio lakini wawili hao hawajawahi kuliweka wazi hilo kwenye public, mtoto pekee wa 50 ambaye anajulikana ana umri wa miaka 16 hivi sasa aliyezaa na Mdada Shaniqua Tompkins.
Mtandao wa TMZ Umefanikiwa kunasa cheti cha kuzaliwa cha Mtoto huyo mpya na kukuta sehemu ya jina la baba imeachwa wazi kitu ambacho kinaweza kutafsiriwa kuwa labda Bi. dada Daphne Joy bado hana uhakika juu ya baba halisi wa mtoto au hakupenda tu kumuweka Fif kwa sababu zake zingine. Lakini mtoto huyo bado anatumia jina lake la mwisho kama Jackson 'Curtis' kitu ambacho tunaamini kuwa Mchizi ni baba halisi wa mtoto. Hadi naiandika story hii 50 bado hajatoa comment yoyote juu ya hili.

0 comments:

Post a Comment