Wednesday, May 30, 2012

Kim Kardashian: NIMEIBIWA MIWANI AMBAYO THAMANI YAKE HAKUNA KITU KINACHOWEZA KUFANANISHWA

 Mwanamitindo,muigizaji,na mjasiria mali,Kim Kardashian, Juzi ijumaa ameibiwa miwani yake iliyokuwa ndani ya begi maeneo ya airpport akiwa anatokea Ufaransa na kudai kuwa hakuna kitu kinachoweza kulipa thamani yake.

Amesema kuwa miwani hiyo ya jua aliachiwa na baba yake Robert Kardashian kabla hajafariki na huwa anayavaa pindi akiwa kwenye matukio maalum tu.
Kupitia akaunti yake ya twitter Kardashian baada ya kugundua ameibiwa ali twit ""Very disappointed in British Airways for opening my luggage & taking some special items of mine! Some things are sentimental & not replaceable."
Pole sana Bi. dada.

Tuesday, May 29, 2012

Nas - Daughters

JUSTIN BIEBER MIKONONI MWA SHERIA KWA KUMSHAMBULIA PAPARAZI

Justin Bieber juzi jumamosi yamemkuta yale yaliyomkuta Diamond platinum wa TZ kwa kumshambulia paparazi kisa mdaku huyo alitaka kumpiga picha.
Kesi hiyo kwasasa ipo mikononi mwa polisi kwa uchunguzi mjini California..

MJOMBA MKUDE: MKALI MWENYE DAMU YA HIP HOP HUYU HAPA

Davis Alfred Mkude a.k.a Mjomba Mkude, ni mkali anayeibukia upande wa muziki wa kizazi kipya atoka na singo ya kwanza iitwayo Sina Pesa.

Mjomba Mkude anasema kuwa hiphop ipo ndani ya damu tangu kitambo na anaamini ataitendea haki siku zote.
Amefunguka kuwa ngoma zipo nyingi na kali zinakuja kutoka kwake hivyo wadau wa hipiT-hiphop wakae tayari.
Kuhusiana na kuchanganya muziki na kazi jamaa ametiririka kuwa kila kitu kina nafasi yake.

Ngoma hiyo ya Sina Pesa imeanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya redio na pia unaweza kuipata kwenye mitandao mbalimbali ikiwemo blog hii.

All the best jombaaa.

Monday, May 28, 2012

Shetta ft Diamond - Nidanganye (Official Video)

Take It To The Head (Explicit)-DJ Khaleed,Rick Ross,Chris brown ,Nicki Minaj & Lil wayne

Nicki Minaj - Right By My Side (Explicit) ft. Chris Brown

MARY J. BLIGE AKWEPA KULIPA DENI BENKI

Malkia na gwiji wa miondoko ya Soul, mdada Mary J. Blige  yupo kwenye wakati mgumu baada ya kuingia kwenye skendo ya kukwepa kulipa deni benki lenye thamani ya dola za kimarekani 250,000 kutokana na mkopo waliochukua mwaka jana kwaajili ya kusaidia maendeleo ya wanawake kupitia foundation yake na Steve Stoute.Benki imesema iliwapasa kulipa deni desemba 2011 lakini hela iliyolipwa ni dola 368.33 tu.

Pia foundation hiyo inashukiwa kwa kutowalipa wasanii kadhaa walioitwa ku 'perform' kwenye 'fund raising' fulani huko mtoni.

MO' CHEDDAH APOTEZA DIRA KWENYE SINGO YAKE MPYA YA 'LOUDER'

Mkali kutoka Nigeria Bi. dada Mo'Cheddah, POP DIVA, Ameonekana kushuka badala ya kupanda katika tasnia ya muziki, hususan baada ya kutoa ngoma yake iitwayo 'LOUDER'.

Kwenye ngoma hii auto tune zimekuwa too much kiasi cha kupoteza ile melody yake ambayo imezoeleka masikioni mwa fans wake.
Kutokana na hayo, wataalamu wa mambo wanatia shaka juu ya ujio wake huo mpya baada ya kimya kingi sana kuwa anaonekana kushuka kiaina.
Ingawa hatuwezi jua lengo la Cheddah,labda keshagundua soko lake jipya.
Video ya ngoma hiyo imefanyika nchini Afrika ya kusini chini ya director Brandon, na humo Mo' ameonekana kwenda nje ya uafrika kitu ambacho kinaweza kupotezea tena umaarufu wake.

Sina pesa-Mjomba Mkude ft.Man Keno (prod...

Gonga hapa umsikie mwana kwa mara ya kwanza kabisa kwa hewa

 Sina pesa-Mjomba Mkude ft.Man Keno (prod... in Hulkshare:

Friday, May 18, 2012

T.I AUNGANA NA JAY-Z KUUNGA MKONO POINT YA OBAMA DHIDI YA NDOA ZA MASHOGA

Rapper Clifford Harris a.k.a T.I ameonesha ku sapoti kauli ya rais Obama juu ya ishu ya kuwepo kwa ndoa za mashoga. Amefunguka hayo alipokuwa akifanya mahojiano na MTV Rapfix.Alipoulizwa anajisikiaje juu ya uwepo wa mpango huo T.I amesema kuwa kwa upande wake sio ishu,ili mradi tu haliingilii mpango wa maisha yake ya kila siku. Amesema kuwa kila mtu anafanya anachojisikia,ilimradi lisimdhuru mtu mwingine.

'Just to speak honestly and being frank, I don’t care… I think that if a matter doesn’t affect your daily life, you shouldn’t take a hard stand on it. If it’s not something that directly affects you, if it doesn’t affect you, then what difference does it make to you what other people are doing with their lives?… I think that you should be able to do whatever you want to do. I don’t see how it matters one way or another’.

T.I amekuwa msanii wa pili kuonesha kuunga mkono point ya Obama, wa kwanza ni Rapa Jay-Z ambaye alitoa wazi sapot yake juu ya suala hilo.

OLA NA CHRIS WAJITOA BIG BROTHER AFRICA STAR GAME

Washiriki wa BBA-STAR GAME kutoka nchini Nigeria wameamua kutangaza kujitoa katika jumba hilo baada ya Ola kulalamikia hali ya afya yake kwa BIGGIE.

Ola amesema kuwa anamatatizo ya shinikizo la damu "blood pressure" na hana hakika kama dawa anazotumia zinamsaidia.
‘Health is wealth", alisema Ola. Yes, this is a game. However, we can’t play with our lives’ aliongezea Chris akiwa katika hali ya huzuni. Wakimaanisha kuwa "afya ni bora kuliko hayo mashindano,na hawapo tayari kuhatarisha maisha yao."
Yote kwa yote kwa upande wangu nadhani hawa jamaa wasingeshiriki kabisa tangu mwanzo kwani walizijua afya zao kabla,so wameziba tu chance za wengine ambao labda wangefanya vizuri. By the way sijaathirika sana kwani watu wangu wa Bongo walishaaga mashindano siku nyiiiingi.

RIHANNA AFUNIKA NDANI YA MOVIE YA BATTLESHIP

Kama unataka kujua kuwa Rihanna ni mkali si kwenye muziki tu hata kwenye Action movie itafute movie iitwayo Battleship uone Bi.dada Rihanna alivyofunika. Ni bonge la movie ambalo hupaswi kuli miss.

DONNA SUMMER a.k.a 'QUEEN OF DISCO' AFARIKI DUNIA

Mkali Donna Summer,Queen of Disco, mmoja kati ya wasanii waliowahi kufanikiwa kimuziki miaka ya 1970's na 1980's amefariki jana ( may 17) akiwa na umri wa miaka 63 kutokana na ugonjwa wa cancer.

Umauti umemkuta akiwa mjini Florida Marekani ingawa bado haijawekwa wazi ni cancer ya aina gani iliyomsababishia kifo.
Habari za kifo chake zimethibitishwa na Muongeaji wa msanii huyo kupitia kituo cha CNN.

R.I.P Queen.

Thursday, May 17, 2012

Lil B KUPIGA MZIGO NA DRAKE

Wiki iliyopita kupitia akaunti yake ya twitter Lil B alionesha nia ya kufanya kazi na mtu mzima Drake wa Young Money, na kwa taarifa tu ni kwamba sasa hivi mpango ushakamilika na ishakuwa confirmed kuwa Lil B na Drake kufanya kazi pamoja.

Waiting....

Black Rhyno ft Suprano - Taking Over ( Official Video)

AliKiba ft Lady JayDee - Single Boy ( Official Video HD )

AliKiba ft Lady JayDee - Single Boy ( Official Video HD )

MKALI WA TENNIS, SERENA WILLIAMS AGEUKIA HIPHOP

Tupa kule tennis kwasasa, mkali wa mchezo wa tennis mwanadada Serena Williams ameamua kuugeukia muziki wa hiphop na kutoa ngoma zake.

Serena amerekodi ngoma kadhaa mwaka jana kutoka katika studio ya the B Major Music Group, Florida ambayo inamilikiwa na rafiki yake ambaye ni mchezaji wa timu ya Baltimore Ravens anayejulikana kama Bryant McKinnie.

Hii ni baadhi ya mistari ya Rap yake mpya:

I ball hard no tennis racket,
I can see these haters through my Gucci glasses,
I make hits like batting practice,
They be like ‘Serena is you really rappin’?’

Thats me, Thanks for listening
Schooling these rappers…

I win, I really mean it,
Swag out this world, you should call me Venus,
That’s my sister, my name is Serena,
I serve ‘em up, no subpoena,
Cook the track up like a frozen pizza”
Duuuuuuu!!!! ametisha

T.I ATANGAZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA YA ' TROUBLE MAN' YENYE TRACK 45

Mkali wa hiphop kutoka ATL, T.I ameweka wazi ujio wa album yake mpya yenye ngoma takribani 45 iitwayo 'TROUBLE MAN'. T.I amefunguka kuwa kwasasa bado yupo kwenye mishemishe za kurekodi album hiyo ila amebainisha kuwa anatarajia kuiachia September 4 mwaka huu.
Ameyasema hayo kupitia mahojiano aliyofanya na Billboard Juice.

Kutokana na wakali ambao watakuwemo ndani ya hiyo albam, ni wazi kuwa itakuwa ni mzigo wa maana.Baadhi ya wakali hao ni Usher, Cee-Lo,Bruno mars na wengine kibaaao.

DMX AFUNGUKA JUU YA UJIO WAKE MPYA KATIKA GEMU

Dark Man X ( DMX) Amesema ameamua kurudi kwenye gemu ya muziki na kuufanya kama kazi.
Amefunguka hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha MTV. Amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na masuala ya kisheria na kupelekea mara kadhaa kutupwa ndani,hivyo kwasasa hataki tena mpango huo. Ametiririka kuwa kwasasa anataka afanye muziki ki professional zaidi na si longolongo.

Kwasasa X ameachia Extended Play 'EP' Yake mpya iitwayo 'The way in EP' kama 'appetizer ' ya album yake mpya ijayo iitwayo 'Undisputed'.

Welcome back X.

Saturday, May 12, 2012

SIKU YA MAMA DUNIANI, UMEJIFUNZA NINI KUTOKA KWA MAMA??

Tarehe 13/05 ni siku maalum kwaajili ya Kina mama duniani, ni siku ambayo tunatakiwa kuonesha ni kwa namna gani Mama amesaidia kukufikisha hapo ulipo. Lakini kuna mambo mengi ya kuangalia katika hii siku. Kubwa ni kuangalia nafasi ya mama kwa mtoto. Je, kina mama wanatimiza wajibu wao wa umama? Na vipi watoto wanatimiza wajibu wao kwa mama?

Asilimia kubwa ya kina mama wa ulimwengu wa sasa wanajisahau na kuwa ni chanzo cha kuharibika kwa watoto. Hii inapelekea ongezeko kubwa la watoto wengi wasio na maadili mema.Kama ndivyo hivyo basi tusisite kuonesha hisia zetu za kuto ridhishwa na malezi ya mama zetu iwapo hawajatimiza wajibu wao ipasavyo hususan kwa siku ya 'MAMA DUNIANI'. Pia tusiwe wachoyo wa shukurani kwa Mama atimizaye wajibu wake.

Na upande wa watoto pia siku hii ni siku muafaka ya kuonesha hisia zako za upendo kwa mama ambaye ndiye hasa aliyekufanya wewe uwepo hapo ulipo,kwani kavumilia mengi yako.

Binafsi nawatakia kina mama wote heri na furaha tele ya siku yenu.

'MTOTO KWA MAMA HAKUI'

Sunday, May 6, 2012

BLACK RHYNO AKAMILISHA KUTENGENEZA VIDEO YA 'TAKIN' OVA'

Mkali wa bongo hiphop Black Rhyno amekamilisha utayarishaji wa video ya ngoma yake ya 'taking ova'. Akiongea na Blog hii amesema tayari ameshakamilisha kilakitu na mzigo anao mkononi tayari kwa kuiweka hewani kwaajili ya fans wake.


Utaiona hii video hapahapa punde.

Saturday, May 5, 2012

BIRD MAN ATANGAZA KUIINGIZA BRAND YA DJ KHALEED 'WE THE BEST' KWENYE 'YMCM' RECORDS

Mkali na  kiongozi wa Young Money Cash Money 'YMCM' Bird man ametangaza rasmi kusaini na kundi la DJ Khaleed 'WE THE BEST' ndani ya YMCM record.

Amefunguka hayo kupitia mahojiano yake na kituo cha MTV na amesema kuwa mpango mzima utaanza na mkali ACE HOOD.All the best YMCM.

MJUE FID Q

Fid Q - Wikipedia, kamusi elezo huru

Fid Q

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Fid Q
Fid Q akionyesha kidole cha shahada - akiashiria wimbo wake wa "Chagua Moja".
Fid Q akionyesha kidole cha shahada - akiashiria wimbo wake wa "Chagua Moja".
Jina la Kiraia Farid Kubanda
Jina la kisanii Fid Q
Nchi Tanzania
Alizaliwa 13 Agosti, 1982
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Mwanamuziki
Ameshirikiana na Juma Nature
Professor Jay
Witness
Mr. Paul
Daz Baba
Langa Kileo
Black Rhino
T.I.D.
Adiri
Ala Sauti
Kampuni Bongo Records
Mj Records
Baucha Records

Farid Kubanda (amezaliwa tar. 13 Agosti, 1982, katika hospitali ya Bugando iliyopo jijini Mwanza) ni msanii wa hip hop na bongo flava kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Fid Q.

Yaliyomo

[hariri] Historia

[hariri] Shughuli za awali (kwa ufupi)

Fid Q alianza shughuli za muziki mnamo miaka ya 1990. Fid Q alitoa kibao chake cha kwanza mwaka 2000 kiitwacho 'Huyu na Yule' ambacho hicho aliimba na msanii Mr Paul. Kibao hiki kilimpa heshima kubwa, kibao hicho kilirekodiwa katika studio za MJ records chini ya usimamizi wake Master Jay mwenyewe.

Kibao chake cha pili kutoka kiliitwa 'Binti Malkia' ambacho alimshirikisha Noorelly. Ilivyofika mnamo mwaka wa 2004 Fid Q alivunja ukimya wake kwa kibao chake mahili kilichokwenda kwa jina la "Fid Q.com", na kibao hicho alikifanya katika studi ya Baucha Records baada ya kuhama kwa MJ.

Kibao hicho kiliirudisha ile hiphop ya Tanzania katika ramani yake halisi na inasemekana hivyo kwasababu kipindi hicho ni kile ambacho wasaanii wengi wa muziki wa kufokafoka walikuwa wamejiingiza katika masuala ya uimbaji kwasababu kulikuwa na uvumi wa kwamba hip hop haikubaliki kwa watu wa Tanzania.

Ilipofika mwezi wa Januri ya 26 katika mwaka wa 2008, Fid Q alipakua kibao kiitwacho "Ni Hayo Tu" alichomshirikisha Prof. J na Langa. Kibao hicho kilibahatika kujinyakulia Tuzo ya Kili kikiwa kama kibao bora cha muziki wa hip hop kwa mwaka wa 2007-2008.

Fid Q ana albamu mbili kwenye soko la muziki. Albamu ya kwanza inaitwa inayoitwa "Vina Mwanzo Kati na Mwisho".[1] Mwishoni mwa mwaka 2009 alitoa albamu ya pili "PROPAGANDA", ambayo imepokelewa vizuri sana Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Mashabiki wa Hip Hop wanaichukulia PROPAGANDA kama ni albamu bora kabisa, yaani 'classic'. Hivi karibuni anategemea kutoa albamu yake ya tatu itakayokwenda kwa jina la "KitaaOLOJIA".

[hariri] Marejeo

[hariri] Viungo vya nje


Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fid Q kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo

Shetta afunga ndoa

Hongera shetta kwa kuvuta jiko ndani, one step ahead.

Thursday, May 3, 2012

SAJUKI YUPO HOI,TUMSAIDIE APATE MATIBABU

Mtayarishaji, muongozaji na mwigizaji mahiri katika tasnia ya filamu, Juma Kilowoko a.k.a Sajuki anahitaji msaada wa shilingi za Tanzania milioni 25 kwaajili ya matibabu yatakayofanyika India. ugonjwa unaomsumbua Sajuki ni kuwa na vivimbe kama matezi katika mishipa ya damu ambayo imekuwa aikiongezeka kila kukicha. Ni wakati muafaka kwetu kumsaidia apate matibabu badala ya kuonesha ufahari mtu akishafariki. Kwa msaada wako fika ofisi za mwananchi. Au soma haya maneno ya kwenye picha hii. Tusaidiane wandugu,leo yeye kesho mimi na wewe. Naamini tukiamua tunaweza kuokoa maisha yake.