Saturday, May 12, 2012

SIKU YA MAMA DUNIANI, UMEJIFUNZA NINI KUTOKA KWA MAMA??

Tarehe 13/05 ni siku maalum kwaajili ya Kina mama duniani, ni siku ambayo tunatakiwa kuonesha ni kwa namna gani Mama amesaidia kukufikisha hapo ulipo. Lakini kuna mambo mengi ya kuangalia katika hii siku. Kubwa ni kuangalia nafasi ya mama kwa mtoto. Je, kina mama wanatimiza wajibu wao wa umama? Na vipi watoto wanatimiza wajibu wao kwa mama?

Asilimia kubwa ya kina mama wa ulimwengu wa sasa wanajisahau na kuwa ni chanzo cha kuharibika kwa watoto. Hii inapelekea ongezeko kubwa la watoto wengi wasio na maadili mema.Kama ndivyo hivyo basi tusisite kuonesha hisia zetu za kuto ridhishwa na malezi ya mama zetu iwapo hawajatimiza wajibu wao ipasavyo hususan kwa siku ya 'MAMA DUNIANI'. Pia tusiwe wachoyo wa shukurani kwa Mama atimizaye wajibu wake.

Na upande wa watoto pia siku hii ni siku muafaka ya kuonesha hisia zako za upendo kwa mama ambaye ndiye hasa aliyekufanya wewe uwepo hapo ulipo,kwani kavumilia mengi yako.

Binafsi nawatakia kina mama wote heri na furaha tele ya siku yenu.

'MTOTO KWA MAMA HAKUI'

2 comments:

  1. Nimeipenda hii, mtoto kwa mama hakui. Happy mother's day

    ReplyDelete
  2. ofcourse uko sahihi

    ReplyDelete