Thursday, May 3, 2012

SAJUKI YUPO HOI,TUMSAIDIE APATE MATIBABU

Mtayarishaji, muongozaji na mwigizaji mahiri katika tasnia ya filamu, Juma Kilowoko a.k.a Sajuki anahitaji msaada wa shilingi za Tanzania milioni 25 kwaajili ya matibabu yatakayofanyika India. ugonjwa unaomsumbua Sajuki ni kuwa na vivimbe kama matezi katika mishipa ya damu ambayo imekuwa aikiongezeka kila kukicha. Ni wakati muafaka kwetu kumsaidia apate matibabu badala ya kuonesha ufahari mtu akishafariki. Kwa msaada wako fika ofisi za mwananchi. Au soma haya maneno ya kwenye picha hii. Tusaidiane wandugu,leo yeye kesho mimi na wewe. Naamini tukiamua tunaweza kuokoa maisha yake.

1 comments: