Tuesday, May 29, 2012

MJOMBA MKUDE: MKALI MWENYE DAMU YA HIP HOP HUYU HAPA

Davis Alfred Mkude a.k.a Mjomba Mkude, ni mkali anayeibukia upande wa muziki wa kizazi kipya atoka na singo ya kwanza iitwayo Sina Pesa.

Mjomba Mkude anasema kuwa hiphop ipo ndani ya damu tangu kitambo na anaamini ataitendea haki siku zote.
Amefunguka kuwa ngoma zipo nyingi na kali zinakuja kutoka kwake hivyo wadau wa hipiT-hiphop wakae tayari.
Kuhusiana na kuchanganya muziki na kazi jamaa ametiririka kuwa kila kitu kina nafasi yake.

Ngoma hiyo ya Sina Pesa imeanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya redio na pia unaweza kuipata kwenye mitandao mbalimbali ikiwemo blog hii.

All the best jombaaa.

0 comments:

Post a Comment