Monday, May 28, 2012

MO' CHEDDAH APOTEZA DIRA KWENYE SINGO YAKE MPYA YA 'LOUDER'

Mkali kutoka Nigeria Bi. dada Mo'Cheddah, POP DIVA, Ameonekana kushuka badala ya kupanda katika tasnia ya muziki, hususan baada ya kutoa ngoma yake iitwayo 'LOUDER'.

Kwenye ngoma hii auto tune zimekuwa too much kiasi cha kupoteza ile melody yake ambayo imezoeleka masikioni mwa fans wake.
Kutokana na hayo, wataalamu wa mambo wanatia shaka juu ya ujio wake huo mpya baada ya kimya kingi sana kuwa anaonekana kushuka kiaina.
Ingawa hatuwezi jua lengo la Cheddah,labda keshagundua soko lake jipya.
Video ya ngoma hiyo imefanyika nchini Afrika ya kusini chini ya director Brandon, na humo Mo' ameonekana kwenda nje ya uafrika kitu ambacho kinaweza kupotezea tena umaarufu wake.

0 comments:

Post a Comment