Tuesday, July 31, 2012

BIFU YA RICK ROSS "FREEWAY" NA RICK ROSS RAPPER " BOSS"

Siku kadhaa zilizopita alijitokeza 'Freeway' ambaye inasemekana ndio mmiliki halali wa jina la 'Rick Ross' na kudai kuwa Rapper Rick Ross 'the boss' wa maybach music, amechukua jina lake na kulitumia bila idhini yake. Hivyo jamaa aliamua kuingia mahakamani kumfungulia Rick Ross 'boss' kesi. Na kubwa analodai Freeway anadai kuwa ingekuwa Rapper huyo 'boss' amepitia maisha kama aliyopitia yeye basi isingekuwa ishu kwake,ila imekuwa tofauti kwani 'Boss'haja experience real life aliyopitia yeye. Katika hatua nyingine,leo hii Freeway ameibuka na kusema kuwa anajitahidi kuwazuia washikaji wake wa karibu ambao wanampango wa kumfanyia kitu mbaya Rapper Rick Ross 'boss' wasifanye hivyo. Moja kati ya washikaji waliotaka kuinunua hiyo kesi ni Suge knight ambaye aliwahi kuwa meneja wa hayati 2pac. Freeway 'RickRoss' ameishi maisha ya kitaa sana na kwake yeye jela ilikuwa kama ndo home. Alikuwa real gangsta & hustler.Fuatilia interview yake aliyoifanya hapo chini.

0 comments:

Post a Comment