Monday, July 16, 2012

RONALDINHO ATOSWA NA COCACOLA BAADA YA KUKUTWA AKINYWA PEPSI HADHARANI

Mkali wa soka kutoka brazil, Ronaldinho 'Gaucho' amemwagwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Cocacola aliyoingia nayo mkataba  wa kuitangaza brand hiyo mara baada ya kupigwa picha akiwa ameshika kopo la kinywaji cha Pepsi likiwa na mrija ambayo ni wapinzani wakubwa wa kibiashara na Coke.
Dinho amekutwa na dhahma hiyo alipokuwa kwenye press conferece na kujikuta aki2pia kitu cha pepsi,na waandishi kama kawaida yao hawakufanya ajizi wakamfotoa mchizi na kumsababishia kumwaga udhamini wa £500,000.
 Ronaldinho hivi karibuni amekuwa kivutio kwa waandishi wa habari kutokana na kuingia kwenye migongano na timu yake aliyokuwa anaichezea ya  Flamengo na kuamua kuingia mkataba na timu nyingine ya  Atlético Mineiro miezi miwili iliyopita.

0 comments:

Post a Comment