Sunday, July 1, 2012

JOHN CENA ATIMIZA MIAKA 10 NDANI YA WWE,AONGELEA MAISHA YAKE

Mkali wa mieleka, John Cena atimiza miaka kumi tangu aanze mchezo huo tarehe 27 June 2002. Kwa kipindi chote hiko cha miaka 10 Cena amekuwa gumzo kwa kila rika kutokana na umahiri wake katika mchezo huo. Amekuwa ni kipenzi na kivutio cha wengi.
Akielezea maisha yake ya mieleka, Cena anaikumbuka mechi yake ya kwanza iliyofanyika June 27 2002 dhidi ya Kurt Angle ambapo anasema kuwa alipata kiraruraru ingawa kwake ndo siku pekee historia ilipoanza andikwa.Kuhusu mafanikio Cena amesema kuwa kuendesha maisha kupitia mchezo huo ndo mafanikio yake. Amesema kuwa hakutarajia hata siku moja kuwa angefikia level aliyofikia leo.

0 comments:

Post a Comment