Saturday, January 19, 2013

Destiny's Child waungana upya, watoa track ya pamoja.

Wanadada watatu waliokuwa wakiunda kundi la Destiny's Child (Beyonce Knowles, Kelly Rowland na Michelle Williams) ambao walitengana miaka kadhaa iliyopita wameamua kulirudisha kundi hilo. Katika kulithibitisha hilo wametoa single ya pamoja mpya iitwayo 'Nuclear' iliyotengenezwa na kuandikwa na Pharrell Williams na kwasasa wanafanyia kazi albam yao mpya ambayo inatarajiwa kuachiwa Januari 29 mwaka huu. Hii inafanana na story ya Juzi niliyoandika ya Kurudi upya kwa kundi la 'Unique Sisterz' la hapa bongo.
Hope ni mwaka mzuri kwa makundi.

0 comments:

Post a Comment