Saturday, January 19, 2013

Rihanna na Chris Brown wapiga collabo ya track nyingine

Chris Brown na Rihanna wamekuwa wakiwaweka mashabiki wao njia panda juu ya mahusiano yao ya kimapenzi. Brizy na Riri walikuwa wapenzi awali, kisha wakatangaza kuachana, lakini siku za hapa karibuni wamekuwa wakionekana wakiwa pamoja na katika pozi za kimapenzi. Na zaidi ya hilo wameweza kushirikiana katika ngoma ya Riri 'Birthday cake'. Then kuna matukio ya picha kadha za utata katika istagram zao zinazowaonesha wapenzi hao kuwa wamerudiana lakini hawataki kutangaza rasmi. Na leo hii Rihanna na Chris Brown wapo studio wakitengeneza ngoma ya pamoja tena iitwayo 'stay'. Katika cover ya track hiyo ambayo ndo hii unayoiona, kwa mbali anaonekana Rihanna akiwa anambusu mtu anaesemekana kuwa ni Brizzy kutokana na tattoo zinazoonekana shingoni. Anyways sio kesi sana, kikubwa ni kuwa huwa wanafanya ngoma kali wakiwa pamoja, na huwa zina hit. All the best Brizzy na Riri.

0 comments:

Post a Comment