Saturday, December 29, 2012
Friday, December 28, 2012
Tuesday, December 25, 2012
Sunday, December 23, 2012
ICE CUBE KUJA NA ALBAM MPYA KABLA YA FILAMU YA 'FRIDAY'
Mkongwe wa N.W.A, Ice Cube, amewataka mashabiki wake wasubiri ujio wa albam yake mpya iitwayo 'Everythang's Corrupt' wakati huku akiendelea kuipika filamu yake ya 'Friday'.
"Yeah, [Last Friday is] coming, "We're marinating on it, putting it together…probably my next album [Everythang's Corrupt] will be done quicker than the Friday movie. We just turned in the script, so it's going to take a couple of more months to put it together."
Ndo mpango wa mkali Ice Cube,na kwenye movie ya Friday anatarajia kumtupia mtu mzima Chris Tucker mkali aliyewahi ku shine kwenye movie za Rush hour.

NAS ATAKIWA KULIPA $MILION 10 KWA KUTOTOKEA KWENYE TAMASHA ANGOLA
December 2011,promota wa American concert,Patrick Allocco alitekwa na mapromota wa Angola baada ya Nas kutotokea kwenye tamasha la mwaka mpya nchini Angola ambapo tayari alishalipwa. Promota huyo amesema kuwa alitekwa ili aweze kuwarudishia mapromota hao kiasi cha pesa zilizotolewa kwaajili ya tamasha hilo. Huku na huku Promota huyo aliweza kuachiwa huru mwezi february 2012. TMZ
inasema kuwa kwamujibu wa sheria promota Alloco amemfungulia kesi Nas kwa madai ya kutaka kulipwa dola za kimarekani milioni kumi ($10,000,000) akidai kuwa kwa siku 50 alizokaa kama mateka ameathirika kisaikolojia,kimwili na kifedha pia.
Kwa upande wake Nas alipohojiwa March 2012 alisema kuwa alitumika kama 'scapegoat' yani mtu anaye hukumiwa au adhibiwa kwa makosa ya wengine. Kesi imefunguliwa Ijumaa juzi tarehe 21 Dec.2012.

Cassidy am Diss Meek Mill kwenye 'Me, Myself & iphone'
Baada ya Meek Mill kusema wazi kuwa ngoma ya Cassidy iitwayo "condom style" ndo ngoma mbaya zaidi katika historia ya Rap, Cassidy nae ametoka na track ya kumdiss Meek iitwayo 'Me, Myself & iphone'.Katika track hii ya Cassidy ameongea mambo kibao
lakini katika verse ya tatu ametupia maneno haya yakimuelekea Meek Mill:
"He said he wanna battle niggas, but when I took him up on his offer he started to reconsider/ That cat lame on every song he rap the same/ That cat changed he got a deal and don't act the same/ That nigga wilding cause he sold a couple hundred thousand/ But I sold triple what that nigga sold my first album/ He not selling cause that nigga can't stop yelling/ He know he can't fuck with you that nigga look up to you/ That ain't nothing new I raised son/ I was around when that clown couldn't even get his braids done/ Why he dropped that 'I'm a Boss' shit?/ Cause his boss say he a BAWSE and he just on his boss dick." Isikilize ngoma hiyo hapa
cassidy-me-myself-iphone
TREY SONGZ AKAMATWA KWA KUMUUMIZA MWANAMKE KWA HELA
Mkali Tremaine Neverson, maarufu kama Trey Songz amekamatwa na kufikishwa polisi kwa kosa la kumuumiza kwa kutumia hela mwanamke mmoja wakati akirusha hela kwa mashabiki kwa staili ya kinyamwezi 'Make it rain'. Kwamujibu wa TMZ Songz alifanya hivyo alipokuwa kwenye party ya kuiachia albam yake mpya siku ya tarehe 21 August. Wakati akirusha hela zimeenda kumgusa machoni mdada huyo na kumsababishia maumivu hasahasa jicho la kushoto,hatimae kwenda kumfungulia mashtaka. Kesi imerushwa hadi Mwezi wa pili.
Saturday, December 22, 2012
FAT JOE AKUTWA NA HATIA YA KUKWEPA KULIPA KODI
Mkali wa Hip hop Fat Joe amekutwa na hatia ya kukwepa ulipaji wa kodi serikalini. Kwa mujibu wa Billboard Mkali huyo amekuwa akiidanganya serikali kwa kipindi cha 2007/2008 zaidi ya kiasi cha $700,000. Kwasasa Joe yupo nje kwa dhamana ya $250,000 akisubiri hukumu mwezi wa nne,ambapo anaweza sota jela kwa kipindi cha miaka miwili.
Wednesday, December 19, 2012
Sunday, December 16, 2012
Wednesday, December 12, 2012
No Name-Hands up
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Muziki wa Bongo, maprodyuza wakali wameungana na kutoa track ya pamoja iitwayo hands up. Wakali hao ambao wanajiita 'No Name' ni P.Funk,Dunga, Lamar,John Mahundi,Akil The brain na Karabani.Dunga ndo kaisimamia beat.
Isikilize ngoma hiyo hapa.Video itakuja soon.
Saturday, December 8, 2012
Tuesday, December 4, 2012
Welcome back Sugu. Atoa ngoma mpya iitwayo ' Hakuna Matata'.
Mkongwe na muasisi katika tasnia ya Muziki wa bongo fleva, Joseph Mbilinyi, maarufu
katika jina la steji kama Mr.II 'Sugu' ametoa track mpya ijulikanayo kama 'hakuna matata'. Mkali huyu ambaye kwasasa ni Mheshimiwa Mbunge ameiachia rasmi ngoma yake hiyo leo hii ikiwa ni harakati za kuwaonesha vijana kazi inavyofanywa.Ngoma imetengenezwa na Ashvin pamoja na Hermy B kutoka studio za B'Hits za jijini Dar. Wel-come back Sugu.
50 Cent Aelezea single yake mpya iitwayo "My life"
Mkali Curtis Jackson, 50 Cent, amejigamba kwa kuielezea single yake mpya ijayo iitwayo "My life" kuwa itakuwa ni single bora kuliko zote alizowahi kutoa. Ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na SOHH. Anaamini kuwa itafanya poa kwani verse ziko tight na Eminem ambae ameshirikishwa kwenye track hiyo ametambaa poa zaidi na midundo ndo usiseme. So ngoja mimi na wewe tusubiri tumsome mchizi Fif. Isikie hapa chini.
50 Cent ft Eminem & Adam Levine - My Life
Ujio Mpya wa Mr. Blue. 'Nipende Kama nilivyo' feat. Walter
Mkali wa Bongo fleva, Young Byser 'Babylon' a.k.a Mr. Blue arudi tena kwenye game baada ya ukimya mrefu, sikia ngoma yake mpya hapa.
P. FUNK 'MAJANI' ASEMA TEKNOLOJIA IMEATHIRI MAUZO YA ALBAM BONGO FLEVA
Unapoongelea muziki wa Bongo Fleva huwezi kuacha kutaja jina la mtayarishaji 'producer' wa muziki huo Paul Mathyse Maarufu kama P. Funk kutoka Studio za Bongo Records. Mkali huyo amefunguka kuwa mauzo ya albamu za muziki huo umeshuka sana kwa hivi sasa. Amebainisha kuwa kipindi cha miaka ya 2001 wasanii walikuwa wakiuza hadi zaidi ya kopi laki tatu,huku akitolea mfano wa albam ya starehe ya Feruz jinsi ilivyofanya vizuri. P. ameweka wazi kuwa sababu kubwa inayosababisha kushuka kwa mauzo ya albam ni kukua kwa teknolojia ya habari ambapo redio stations zinazo piga muziki huo sikuhizi zimekuwa nyingi, mitandao ya kijamii ikiwemo You tube n. k. hivyo msikilizaji anaweza kupata muziki wowote anaouhitaji kwa muda wowote kuliko zamani ambapo wasikilizaji wengi walikuwa wakitegemea tapes. Kwa upande wake anaona kuwa teknolojia inasaidia kuwasogeza wasikilizaji hivyo kutanua soko la muziki.
Mkali P. Funk ameyasema hayo leo kupitia mahojiano yake aliyofanya katika kipindi maarufu cha XXL cha Clouds FM katika segment ya 255.
Mkali P. Funk ameyasema hayo leo kupitia mahojiano yake aliyofanya katika kipindi maarufu cha XXL cha Clouds FM katika segment ya 255.
Sunday, December 2, 2012
Saturday, December 1, 2012
EVE AFUNGUKA,ASEMA STEVIE J. NDO ALIKUWA MPENZI WAKE WA KWANZA
Mwanadada mkali wa Hiphop kutoka States,Eve, amefunguka kuwa Star kutoka ATL,Stevie J. ndo alikuwa mpenzi wake wa kwanza kabisa. Amebainisha hayo kupitia kipindi cha Mdada Angie Martinez wa kituo cha Hot 97 Jumatano iliyopita.
Kwasasa Eve ana promote albam yake mpya iitwayo 'Lip Lock'ambayo inatarajiwa kuachiwa Mwezi wa nne mwaka huu.Eve aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Stevie J. ktambo enzi za Ruff Ryders ambapo aliingia kwenye skendo la kutengeneza mkanda wa ngono akiwa na mchizi huyo. Lakini Eve ansema kwasasa hayo yamepita so ana focus zaidi kwenye kazi zake, na tayari keshaachia ngoma kadhaa kwenye albam hiyo ukiwemo wimbo wa 'she bad,bad'
Fuatilia Interview aliyoifanya na Angie Martinez Hapa chini.
B.O.B ASEMA HAKUWAHI KUPATA SUPPORT YA MSHUA WAKE
Mkali kutoka Atlanta (ATL), B.O.B ameweka wazi kuwa katika harakati zake za kuingia katika Rap hata siku moja hajawahi kupata support kutoka kwa baba yake. Akiongea katika episode ya hivi karibuni ya MTV iitwayo "This Is How I Made It," mchizi amesema kuwa mshua wake alikuwa hajavutiwa na chaguo la mwanae la kazi hiyo. "I remember I was walking through the house with a rap book, a do-rag on
and some headphones or something, and my dad stopped me," he said,
recalling one pivotal moment. "He was like, 'Why are you trying to be
something that you're not?' " Alisema Bobby Ray. Kisha jama alimjibu mshua kuwa 'What do you mean, something I'm not?' I'm an MC, I' m a lyricist, I'm a rapper — I love this. Yeah habari ndo hiyo,pale unapoamua kufanya kitu ukipendacho then familia haipo upande wako.Licha ya kutokuwa na support hiyo mchizi alikaza na hatimaye kuwa hot hivi sasa.
Thursday, November 29, 2012
Tuesday, November 27, 2012
SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI
Yule mkali wa sanaa ya vichekesho na bongo fleva Hussein Ramadhani Mkieti,maarufu kama Sharo milionea amefariki dunia jana majira ya saa mbili usiku katika kijiji cha Lusanga-muheza,Tanga kutokana na ajali ya gari iliyotokea akiwa njiani akielekea nyumbani kwao Muheza.
akitokea Dar ea salaam. Kamanda wa Tanga Bwana Costantine Masawe amethibitisha kutokea kwa kifo cha msanii huyo. Kamanda Masawe amesema ajali imetokea baada ya gari dogo lenye usajili na. T478 BVR Toyota Harrier lililokuwa linaendeshwa na marehemu kuacha njia na kuingia mtaroni na kusababisha umauti huo. Mpaka sasa mwili upo hospitali teule ya muheza Tanga na mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano wiki hii. R.I,P Sharo Milionea, we realy Gonna mic u Bro.

Monday, November 26, 2012
Friday, November 23, 2012
Monday, November 19, 2012
SNOOP DOGG ATAKA KUINUNUA CELTIC NA KUMSAJILI BECKHAM
Mkongwe na mkali wa Rap kutoka nchini Marekani, Snoop Dogg ameweka wazi nia yake ya kununua hisa ya klabu ya mpira wa miguu ya Celtic ya Uingereza. Snoop ambaye amewahi kupigwa marufuku kuingia nchini uingereza kutokana na makosa yanayohusishwa na madawa ya kulevya na matumizi ya silaha za moto, ameweka wazi kuwa ameshafanya mazungumzo na rafiki yake kiungo mkali wa LA Galaxy David Beckham ili akipige katika klabu yake pindi akikamilisha taratibu. Snoop amefikia wazo hilo baada ya kuvutiwa na kocha wa Celtic, Neil Lennon, mara baada ya kuichapa Barcelona kwenye mashindano ya klabu bingwa ulaya yanayoendelea. "Sio kitu kipya kwa supastaa wa hiphop kuwekeza kwenye michezo,lakini ni kitu kipya kwa supastaa wa hiphop kuwekeza kwenye football" alisema Snoop kupitia 'The Scottish Daily Record'. Kwaupande wangu naona ni bonge la wazo kwa mkali huyu. All the best bro.
Saturday, November 17, 2012
Thursday, November 15, 2012
Sunday, November 11, 2012
Thursday, October 18, 2012
Wednesday, October 17, 2012
Tuesday, October 16, 2012
Monday, October 15, 2012
Tuesday, September 25, 2012
Thursday, September 13, 2012
Saturday, September 8, 2012
COLLINS 'MO LOVER' KICHWA KIPYA BONGO, ATOKA NA "NILIKUPENDA"
Kutoka studio ya AM Records chini ya mhunzi wa sauti Manecky, anapatikana mchizi huyu hapa Collins a.k.a Mo'Lover akiwa amemshirikisha Drama boy wamedondosha ngoma kali ambayo kwangu mimi naona kama ni 'Good Start n good staff'.Baada ya kunitumia hii ngoma nikaona ni vyema nikikudondoshea na wewe uisikie kisha ujipakulie.
Thursday, September 6, 2012
Wednesday, September 5, 2012
Sunday, September 2, 2012
Saturday, September 1, 2012
MR. FLAVOUR ABURUZWA MAHAKAMANI NA WAGHANA KWA WIZI WA WIMBO
Mkali kutoka Nigeria Flavour N'ababia maarufu kama Mr. Flavour ameburuzwa mahakamani na wasanii ktuka Ghana wajulikanao kama Wutah kwa tuhuma za kuiba wimbo wao wa mwaka 2008 uitwao 'Kotosa'. Kwa mujibu wa waghana hao 'Wutah' wameutaja wimbo mpya wa Flavour uitwao 'kwarikwa' kuwa ni 'kopi' ya wimbo wao uitwao 'kotosa' ambao
waliuachia hewani 2008. Wanamtuhumu Flavour kwa kuiba chorus,rhythm na tempo ya wimbo wao huo bila idhini wala makubaliano yoyote.Meneja wa Flavour, Benjamin, amekataa kuongea chochote juu ya tuhuma hizo kwasasa. Flavour ambaye Jina kamili ni Chinedu Okoli, kwasasa yupo chini ya 2nite entertainment. Hapa chini ni video yake ya 'kwarikwa' akimshirikisha Fally ipupa.
Jaribu kuzitofautisha hizi ngoma hapa chini
WUTAH KOTOSA
Sunday, August 26, 2012
Friday, August 24, 2012
B.O.B NA NICKI MINAJ WAMETISHA KWENYE VIDEO YA 'OUT OF MIND'
Wakali B.O.B na Nicki Minaj wametisha ilembaya katika video ya 'Out Of Mind'ambapo inaanza kwa kumuonesha Bobby ray akiwa amefungwa na amevishwa mavazi ya wagonjwa wa akili,na kupitia kamera za usalama za hospitali anaonekana bob akipiga ukuta huku
akijitahidi kuyatoa mavazi meupe aliyovalishwa, katika kipande kingine mchizi anasikika aki rap maneno haya "Don't look at me wrong, I'm out of my mind, Nostradamus and da Vinci combined/ So paranoid of espionage, I'm watchin' my doors and checkin' my blinds," kisha kama bahati hivi B.O.B anapata rafiki ambaye ni Dokta Minaj Nicki, na wakati wa mahojiano ya mgonjwa na dokta, minaj analitoa koti lake jeupe na kuanza ku rap maneno akimwambia Bob "You gonna really need a wish right now when my goons start shootin' stars."
Ni bonge ya video ambayo hupaswi kuikosa kuiona na ndio maana nimekutupia hapa chini uichukue. Enjoy.
Thursday, August 23, 2012
'FREELANCERS' MOVIE MPYA YA 50CENT
Saturday, August 18, 2012
Friday, August 17, 2012
RICK ROSS AACHIA 'AMSTERDAM' VIDEO
Rapa Rick Ross ameachia video mpya kutoka katika albam yake mpya iitwayo 'God forgives,I dont'.
Wimbo unaitwa 'Amsterdam' na video imeongozwa na Dre films. Humo ndani wamo wakali kadhaa kama vile Tyga na Omarion. Alipokuwa akiongelea video hiyo Rossy ambaye pia ni Boss wa MMG amefunguka kuwa video ime base katika 'red light district', na alipoulizwa ni kwanini ime base huko alifunguka kama ifuatavyo: ‘I kinda flipped it where being a boss you gotta get approval for a greenlight’.
‘I’m one of those people you can’t
green light. As long I’ve been in this game, there’s been a lot of talk,
but ain’t nobody stepped on these 11 and a half’s. The reason being:
This is the red light district, you can’t move on this side.’ Ni bonge moja la video. Itupie jicho hapa chini.
HATIMAYE ROBIN VAN PERSIE KUTUA OLD TRAFORD
Inaonesha Babu Ferguson ameshinda mbio za kumchukua RVP, na kwa mantiki hiyo mchezaji huyo anatarajiwa kukipiga na mashetani wekundu na kuachana na Arsenal.Kweli chema chajiuza. All the best RVP.
Thursday, August 16, 2012
NICKI MINAJ AMFAGILIA FOXY BROWN,ASEMA NDIYE PEKEE ALIYEMVUTIA KUINGIA KWENYE GAME
Mwanadada Nicki minaj kutoka YMCMB ameweka wazi kuwa msanii pekee aliyemfanya avutike kwenye game la muziki ni mwanadashosti Foxy Brown.
Ameyasema hayo alipokuwa kwenye steji na kumpandisha stejini Foxy kisha kufunguka live kuwa Foxy ndiye msanii pekee aliye mu-influence kwenye game hii ya hip-hop. Wakiwa stejini Minaj alisikika akimpa asante Foxy kwani ndiye aliyemfanya awepo hapo alipo "I really wanna thank you for being one of my biggest influences in the game,""For her to be on my stage, it was emotional, and she was emotional," "This is what this is really about. When you get where you have arrived to, you give thanks to people who opened those doors and triggered something in your mind. When I found out Foxy Brown was from Trinidad, that did something to me. In my mind, I felt like I could be proud of where I'm from." Alisema Nicki.

DRAKE NA CHRIS BROWN WAPIGWA FAINI YA DOLA MILIONI 16
Wakali Drake na Chris Brown wamepigwa faini ya dola za kimarekani milioni 16 Kutokana na ugomvi kati yao uliotokea Juni 14 mwaka huu na kusababisha takribani watu 7 kuumizwa.
Washikaji wamekumbwa na faini hii jumatano jana baada ya mahakama kuona kuwa wanastahili kulipa kutokana na hasara iliyotokea usiku wa tukio katika klabu ya W.I.P.
Washikaji wamekumbwa na faini hii jumatano jana baada ya mahakama kuona kuwa wanastahili kulipa kutokana na hasara iliyotokea usiku wa tukio katika klabu ya W.I.P.
The Expendables 2, KUZINDULIWA RASMI KESHO
Ni bonge la movie ambalo kwa mpenda action huwezi kuthubutu kuikosa. Inajumuisha wababe kibao akiwemo Sylvester Stallone 'Rambo', Jean Claude Van Damme, Jason Stathan, Chuck Norris na wakali wengine kibao.
Mpango mzima unazinduliwa kesho na baada ya hapo ni sokoni kama kawa tujibebee kopi.
Mpango mzima unazinduliwa kesho na baada ya hapo ni sokoni kama kawa tujibebee kopi.
Sunday, August 12, 2012
NEY WAMITEGO NA SINTA NDANI YA BIFU
Juzi kati kupitia kipindi cha runinga cha Clouds tv kiitwacho Take One ambacho kime base zaidi katika kufanya mahojiano na masupastaa wa bongo movie, kilikuwa meza moja na mkali wa bongo flavour Nay wamitego, ambaye katika single yake iitwayo 'Nasema nao'amewachana mademu wa bongo movie kavukavu kuwa wengi wao ni malaya.
Nay ameenda mbali zaidi baada ya kumtaja live mwanadada Christina a.k.a Sinta kuwa ni mmojawapo ya wasanii ambao wako tayari kufanya kitu chochote ilimradi aweze kung'ara tena katika gemu.
Baada ya kutajwa na Nay, Mdada Sinta naye kupitia mtandao wake ameamua kujibu kwa kumchana kavukavu mchizi Nay.Swali langu ni kwamba, hivi ni sawa kwa wasanii kupakana live kihivi?
KAAAAAAZI KWELI KWELI.
Hii stori ni kwa msaada wa DJ Fetty
RIHANNA AFUNGUKA KWA OPRAH WINFREY JUU YA CHRIS BROWN, ASEMA AMEPOTEZA 'BEST FRIEND'
Mwana da-shosti Rihanna amefunguka kupitia kipindi cha mwanamama Oprah Winfrey kuwa kutokana na kutengana kwake na mkali Chris Brown anahisi kama amempoteza rafiki wake kipenzi 'best friend'.
Rihanna kwenye mahojiano hayo anaonekana kutosita kuonesha hisia zake juu ya Chris Brown.
Kutokana na hayo watabiri wa mambo wanahisi wapenzi hawa wa zamani Chris na Rihanna kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kurudiana.
Hii ni Teaser kutoka kwa Mwanamama Oprah juu ya Next Chapter ambayo itaenda hewani kuanzia August 19.
Hii ni Teaser kutoka kwa Mwanamama Oprah juu ya Next Chapter ambayo itaenda hewani kuanzia August 19.
Tuesday, August 7, 2012
MWANDISHI WA HABARI MOHAMED MASENGA, AINGIA KWENYE SIASA KISARAWE
Mwandishi wa habari, Mohamed Masenga, ameamua kubadili upepo na kuanza kujishughulisha na mambo ya kisiasa. Mwandishi huyo ameonekana akichukua fomu ya kugombea nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu UVCCM Taifa ( NEC ) pande za kisarawe. Kama inalipa all the best kaka. Siasa njema.
MUWEZESHE 'CATRINA' FIESTA SUPA NYOTA 2012
Tuma neno FIESTA 14 kwenda namba 15678 kumpigia kura Catrina ashinde katika fiesta supa nyota 2012.Ni mdada mkali wa sauti kutoka A-town. Anaweza.
Thursday, August 2, 2012
Tuesday, July 31, 2012
BIFU YA RICK ROSS "FREEWAY" NA RICK ROSS RAPPER " BOSS"
Siku kadhaa zilizopita alijitokeza 'Freeway' ambaye inasemekana ndio mmiliki halali wa jina la 'Rick Ross' na kudai kuwa Rapper Rick Ross 'the boss' wa maybach music, amechukua jina lake na kulitumia bila idhini yake. Hivyo jamaa aliamua kuingia mahakamani kumfungulia Rick Ross 'boss' kesi. Na kubwa analodai Freeway anadai kuwa ingekuwa Rapper huyo 'boss' amepitia maisha kama aliyopitia yeye basi isingekuwa ishu kwake,ila imekuwa tofauti kwani 'Boss'haja experience real life aliyopitia yeye.
Katika hatua nyingine,leo hii Freeway ameibuka na kusema kuwa anajitahidi kuwazuia washikaji wake wa karibu ambao wanampango wa kumfanyia kitu mbaya Rapper Rick Ross 'boss' wasifanye hivyo. Moja kati ya washikaji waliotaka kuinunua hiyo kesi ni Suge knight ambaye aliwahi kuwa meneja wa hayati 2pac.
Freeway 'RickRoss' ameishi maisha ya kitaa sana na kwake yeye jela ilikuwa kama ndo home. Alikuwa real gangsta & hustler.Fuatilia interview yake aliyoifanya hapo chini.
KWETU STUDIO YAACHIA SOUNDTRACK YA 'MAISHA SAFARI' YA ERIC MRINDIMA
Hii ni soundtrack ya movie mpya iitwayo 'Maisha safari' inayochezwa na mkali Eric mrindima ambayo ipo jikoni chini ya Muongozaji Mussah Msafiri 'the travellah' wa Kwetu studio. Stay tuned kwa hili.
Saturday, July 28, 2012
Tuesday, July 24, 2012
Saturday, July 21, 2012
HATIMAYE MARIAH CAREY AKUBALI DILI LA KUWA JAJI WA 'AMERICAN IDOL'
Mariah Carey ameonesha kukubali kusaini dili la kuwa jaji wa American Idol. Kwasasa wapo katika hatua za mwisho za kusaini dili hilo. Imewekwa wazi kuwa kama itaenda poa Carey ataweka kibindoni kiasi cha dola milioni 17 za kimarekani ($17 million) kwa msimu mmoja.
Ni siku kadhaa blog hii iliandika kauli ya Nick Cannon ambaye ni Mume Mariah carey akisema kuwa ili kumpata Carey awe jaji ni lazima American idol watoe mzigo wa kutosha, so nadhani wamemsikia. Hongera Carey.

Thursday, July 19, 2012
Wednesday, July 18, 2012
Monday, July 16, 2012
VUNJENI BENKI ILI KUMPATA MARIAH CAREY AMERICAN IDOL,ASEMA NICK CANNON
"Kama American Idol inamuhitaji Mariah Carey kuwa mmoja wa majaji wao ni lazima wavunje benki" hii ni kauli ya Mr. Carey, Nick Cannon akiongelea point ya Mariah carey,mkewe kuwa mmojawapo wa majaji wa American idol msimu ujao kutokana na waliokuwa majaji Jennifer Lopez na Steven Tyler kutangaza kuwa hawatakuwepo kwenye jopo la majaji msimu ujao. Kauli hii ya Nick inatokana na ukweli kuwa American idol imekuwa haina malipo mazuri kwa majaji wake.
Yap, vipi kibongobongo??????/
Yap, vipi kibongobongo??????/
BAADA YA 'AMEN' YA MWANA FA, Chukua na hii ' AMEN' - MEEK MILL ft. DRAKE
Hii ni official video ya mkali kutoka Maybach Empire,Meek Mill akimshirikisha Drake kutoka YMCMB. Ngoma inaitwa 'Amen', ni siku kadhaa Mwana FA nae ametoa ngoma ikiitwa 'amen' hivyohivyo, Inakuaje idea zinagongana???? Anyways, yote maisha.
RONALDINHO ATOSWA NA COCACOLA BAADA YA KUKUTWA AKINYWA PEPSI HADHARANI
Mkali wa soka kutoka brazil, Ronaldinho 'Gaucho' amemwagwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Cocacola aliyoingia nayo mkataba wa kuitangaza brand hiyo mara baada ya kupigwa picha akiwa ameshika kopo la kinywaji cha Pepsi likiwa na mrija ambayo ni wapinzani wakubwa wa kibiashara na Coke.
Dinho amekutwa na dhahma hiyo alipokuwa kwenye press conferece na kujikuta aki2pia kitu cha pepsi,na waandishi kama kawaida yao hawakufanya ajizi wakamfotoa mchizi na kumsababishia kumwaga udhamini wa £500,000.
Ronaldinho hivi karibuni amekuwa kivutio kwa waandishi wa habari kutokana na kuingia kwenye migongano na timu yake aliyokuwa anaichezea ya Flamengo na kuamua kuingia mkataba na timu nyingine ya Atlético Mineiro miezi miwili iliyopita.

KANYEWEST & KIM KARDASHIAN WAISHI KAMA MAPACHA HIVI SASA
Kanyewest na Mpenzi wake Kim Kardashian hivi sasa wanaishi kama mapacha vile.
Hii ni kutokana na namna ya mienendo yao kufanana kwa siku kadhaa mfululizo. Hivi sasa kim na kanye wakitoka wanavaa nguo zinazo fanana rangi,muda wote wapo pamoja wakishikana mikono. Kila umuonapo Kim basi na Kanye yupo. Hiyo imepelekea kubatizwa jina la 'Kimye',ikimaanisha kim na kanye.
Ofkouz inapendeza, all the best 'Kimye'.

Sunday, July 15, 2012
MICHAEL SCOFIELD,MKALI WA 'PRISON BREAK'
Ofcourse, nani asiyezijua series za Prison break? Ni series ambazo ni kali na nathubutu kusema kuwa hazichoshi hata kuzitazama.
Star wa series hizo ,Michael Scofield hasa ndo ambaye ameweza kuziweka katika umaarufu huo kutokana na umahiri anaouonesha mle ndani. Kwa upande wangu mimi nampa heshima michael popote alipo. Kwa wasanii wachanga kunamengi ya kujifunza kutoka kwake.

MTOTO WA RAMBO AFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 36,
Mtoto wa kiume wa Star wa movie za kibabe,Sylvester Stallone (RAMBO) aitwaye Sage Stallone, amefariki juzi Trh 13/07/2012 akiwa na umri wa miaka 36.
Sababu za kifo chake bado hazijafahamika wazi ingawa ripoti za awali zinaonesha kuwa alikuwa nyumbani kwake na girlfriend wake au mfanyakazi wake wa ndani.Baada ya watu wa afya kuja pale wamesema kuwa kifo kimesababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya,ingawa bado haijathibitishwa zaidi juu ya hilo.
Sage alishawahi kucheza filamu na baba yake iitwayo Rocky 5.

Thursday, July 12, 2012
NAOMI CAMPBEL KUDONDOKA TZ KUSAKA VIPAJI VYA UREMBO
Naomi atatua bongo kufuatia ziara yake ya Afrika ya kusaka vipaji. Hope itakuwa ni chance nzuri kwa wadada wenye ndoto za kufanya poa katika tasnia hiyo hapa TZ. So itumieni hiyo chance wadada coz najua mabinti wa kibongo ni wakali.
Friday, July 6, 2012
KANYE WEST KUACHIA ALBUM MPYA,PRODUCER WAKE AFUNGUKA
Producer huyo amesema kuwa fans wa Kanye wakae tayari kupata album hiyo ikiwa ni kama double dose kwani album yake ya 'summer cruel' bado ipo sokoni.
No I.D amesema wapenzi watarajie vitu bomba.
Wednesday, July 4, 2012
SHILOLE KU- SHOOT VIDEO MPYA,KWETU STUDIO YAHUSIKA
Mdada mwenye vipaji kibao vikiwemo vya muziki na uigizaji Shilole,kufanya video ya wimbo wake uitwao VIUNO TUCHEZE ambao amewashirikisha richard mavoko na kitokololo. .
Video hiyo inatarajiwa kufanywa na studio inayokuja juu katika utengenezaji wa video kali,Kwetu studio iliyopo DSM.
Video hiyo inatarajiwa kufanywa na studio inayokuja juu katika utengenezaji wa video kali,Kwetu studio iliyopo DSM.
ERIC MRINDIMA,MKALI WA COMEDY, KUJA NA 'MAISHA SAFARI'
Mkali wa Comedy Eric Mrindima,ambaye bado anandoto za kufanya mengi
mazuri anatarajia kuachia 'short film' yake iitwayo "Maisha safari".
Mpango huo unasimamiwa kwa karibu na Kwetu studio ya Jijini Dsm.
Hizi ni baadhi ya picha zilizopigwa wakati wa harakati za upikaji hiyo kitu.
Hope itakuwa poa, ngoja tuisikilizie.
Hizi ni baadhi ya picha zilizopigwa wakati wa harakati za upikaji hiyo kitu.
Hope itakuwa poa, ngoja tuisikilizie.
Subscribe to:
Posts (Atom)